Historia

Historia ya Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha TAZARA Mbeya SACCOS LTD

Chama cha Ushirka wa Akiba na Mikopo cha Tazara Mbeya kilianzishwa Mwaka 1992 kikiwa na Wanachama waanzilishi 123 na Mtaji wa Tshs 600,000/= Chama kilipata Usajili rasmi mnamo tarehe 20.10.1994 kwa namba ya kuandikishwa MBR 349.

Hadi sasa chama kina jumla ya Wanachama 1,300 ambapo Wanaume ni 1000 na Wanawake 275 na Vikundi vya Wajasiriamali 25. Idadi ya Wanachama imeendelea kuongezeka siku hadi siku. Chama pia kinatoa huduma ya kuweka Amana (Current Account). Wateja wanaofungua akaunti za Amana wamefikia 2,000. Akaunti za Amana zinazofunguliwa katika Chama chetu hazina makato ya kila Mwezi hivyo huwasaidia sana Wajasiriamali wadogo, Vikundi/Vikoba, Wafanyakazi na Wananchi kwa ujumla kuweka Amana zao kwa faida.

Chama kina jumla ya Mtaji wa Tshs 4.5 Bilioni ikiwa ni Hisa za Wanachama zenye thamani ya Tshs 680 Milioni wakati Akiba na Amana za Wanachama ni Tshs 3.8 Bilioni.

Huduma kuu zitolewazo na Chama ni kuweka Akiba za Wanachama na kutoa Mikopo kwa riba nafuu na endelevu. Chama pia kinapokea na kutoa Amana za Wanachama na Wananchi waliopo karibu na eneo la Iyunga ziliko ofisi za Chama. Tazara Mbeya Saccos Ltd imeendelea kupanua wigo wa huduma zake ambapo sasa inatoa huduma za uwakala wa Mitandao ya Simu kama:- M-PESA, tiGO-PESA, AIRTEL MONEY, HALLO PESA na Uwakala wa Mabenki mbalimbali kama vile:- NMB, CRDB na EQUITY Benki.

Tazara Mbeya Saccos Ltd ni taasisi inayotoa huduma kwa wanachama ambao ni waajiriwa wa Shirika la Reli, TAZARA na Wajasiriamali wa Vikundi na Mjasiriamali mmoja mmoja wanaopatikana maeneo ambayo yapo karibu na reli ya TAZARA. Eneo la shughuli za Chama ni maeneo ya mikoa yote inayopitiwa na Reli ya TAZARA ambayo ni:- Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Iringa, Njombe, Mbeya na Songwe. Makao makuu ya Chama yapo Jijini Mbeya.