MIKOPO

Huduma ya Mikopo itolewayo na Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Tazara Mbeya SACCOS LTD

AINA YA MIKOPO ITOLEWAYO NA MASHARTI YAKE

1. Mikopo ya Maendeleo:-

(a). Mikopo ya Maendeleo ambayo Mwanachama atakopa mara mbili ya kiwango cha akiba alichochangia, ili kuinua kipato kwa ajili ya familia kama vile kujenga nyumba, kununua shamba, Ng’ombe wa maziwa, kufuga Kuku n.k.

(b). Riba ya mkopo wa maendeleo itakuwa asilimia 1.2 kwa salio nyoofu (Straight line).

(c). Kiwango cha mkopo wa Maendeleo kitakuwa kuanzia Tshs 1 - 20,000,000/=.

(d). Mkopo wa Maendeleo kuanzia Tshs 1/= hadi 5,999,999/= hautalipiwa ada

(e). Mkopo wa Maendeleo kuanzia Tshs 6,000,000/= mpaka 20,000,000/= utalipiwa ada ya 1% na pia Mkopaji atatakiwa kuwa na hisa zisizopungua asilimia tano ya mkopo uliochukuliwa.

(f). Mikopo inayozidi kiwango cha Tshs 10,000,000/= pamoja na kulipiwa ada ya 1% pia itakatiwa bima ya 1.8% ya kiwango cha Mkopo uliyochukuliwa.

(g). Mkopo unaozidi Tshs 10,000,000/= kabla ya kuchukua mkopaji atasaini Mkataba na kuupeleka kwa wakili anayetambulika kiserikali.

(h). Mikopo yote inayozidi kiwango cha Tshs 10,000,000/= pamoja na kusaini Mkataba pia dhamana ziliozowekwa kwa ajili ya Mkopo mf: nyumba, kiwanja hati zake zitaletwa chamani kabla yakutolewa mkopo.

(i). Kwa Mteja anayekopa kiasi kinachozidi milioni kumi hadi milioni ishirini, Dhamana isiyohamishika ni lazima iwe yake au Mdhamini wake.

(j).Dhamana yaweza kuwa Leseni ya Makazi, Hati ya kiwanja au Nyumba, Hati ya kuthaminisha Kiwanja au Nyumba.

2. Mikopo ya dharura:-

(a). Mikopo hii itatolewa kwa Mwanachama anapokuwa amepata matatizo na anahitaji msaada wa haraka mfano kifo, na majanga mengine yatakayothibitishwa na Afisa Mikopo, kiwango cha mkopo Tshs 300,000/=.

(b). Riba ya mkopo huu itakuwa asilimia tatu kwa salio la nyoofu (straight line).

(c). Muda wa Marejesho utakuwa miezi minne.

(d). Mdhamini mmoja ni lazima.

3. Mikopo ya Vifaa:-

(a) Mikopo hii itahusu vifaa mbali mbali kama Bati, Cement, Redio, TV, Pikipiki, Sola, Jiko la gesi kwa mwanachama ambaye ataonekana ana uwezo wa kulipa.

(b).Ukomo wa Mikopo ya Vifaa utakuwa Tshs.1,000,000/= isipokuwa mikopo ya pikipiki hautazidi Tshs 2,000,000/= na sola itakuwa ni vitu halisi na mwanachama atatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:

(i). Awe na Akiba isiyopungua Tshs 700,000/=.

(ii). ii Asiwe na mikopo zaidi ya miwili kati ya ifuatayo: Biashara, Maendeleo, Payroll na Elimu.

(c). Mikopo ya vifaa inayozidi Milioni moja itaambatana na profoma invoice ambayo itaonyesha hali halisi ya kifaa kinachonunuliwa.

(d). Riba yake itakuwa asilimia 3 kwa salio la Mstari mnyoofu.

(c). Muda wa marejesho ya mkopo usiozidi Tshs 1,000,000/= ni miezi 12 na Mkopo unaozidi Milioni moja ni miezi kumi na nane.

4. Mkopo wa Marekebisho ya deni:-

(a). Mkopo huu utatolewa kwa Mwanachama ambaye Mkopo alionao kwenye Chama amerejesha kiwango cha kufikia asilimia 70.

(b). Riba yake itakuwa bakaa ya riba ya MKOPO na itakatwa mara moja anapopewa mkopo.

(c). Mikopo ya marekebisho itakuwa ni mikopo ya Maendeleo na Dharura tu.

5. Mikopo ya Elimu:-

(a). Mikopo hii itatolewa mara mbili kwa mwaka yaani Januari na Julai, kufuatana na Mihula ya Shule. Kiwango cha juu cha kukopa kitakuwa Tshs.1,000,000/= kwa muhula mmoja.

(b). Mwombaji wa Mkopo huu ataeleza kama mkopo anaoomba ni wa Elimu ya Msingi, Sekondari au Chuo.

(c). Mikopo yote ya Elimu itapitishwa kwa pamoja lakini malipo yatafanyika kwa kufuata mihula ya Elimu ya Msingi, Sekondari au Vyuo.

(d). Mikopo ya Elimu ya juu itazingatiwa kwa wakati husika.

(e). Riba yake itakuwa asilimia 2% kwa salio nyoofu(straight line)

(f). Muda wa Marejesho ni Miezi sita.

6. Matangulizo ya mshahara(SALARY ADVANCE):

(a).Mwanachama anaweza kuomba matangulizo ya mshahara kwa kiwango cha asilimia mia moja mara tu baada ya payroll za mwezi husika zitakapokuwa zimekifikia Chama. Na kabla ya payroll kufika Mwanachama ataruhusiwa kuchukua kiwango cha Matangulizo ya mshahara kisichozidi Tshs.100,000/=. Matangulizo ya mshahara yatakatwa yote kwenye mshahara wa mwanachama kwa mwezi husika.

(b).Mkopo huu utaidhinishwa na afisa mikopo na kuthibitishwa na Meneja.

(c).Riba yake itakuwa asilimia 5% kwa salio nyoofu (Straight line).

7. Mikopo ya Biashara:-

(a).Mikopo ya Biashara itakopeshwa kwa mwanachama ambaye tayari anayo biashara au anayetaka kuanzisha, kwa kuleta mchanganuo ambao utaonyesha biashara anayofanya au anayokusudia kufanya. Kabla ya chama hakijatoa mkopo wa Biashara Afisa mikopo atafika na kuona eneo la biashara lilipo au inapokusudiwa kunzishwa.

(b). Mikopo ya Biashara kwa vikundi wanachama dhamana zao zitakuwa:

(i). Akiba za kikundi husika

(ii). Miradi yenyewe kupitia biashara akaunti.

(ii). Hati ya mali isiyohamishka mfano: Nyumba au kiwanja chenye hati miliki zilizo thibitishwa na Mwanasheria.

(c). Riba yake itakuwa asilimia mbili kwa salio nyoofu(straight line) kwa mkopo kuanzia Tshs 20,000,001 - 50,000,000/=.

(d). Mkopo wa Biashara utalipiwa ada ya 1.5% na bima 1.8 % kama kinga ya awali ya mkopo.

(e). Mikopo yote ya Biashara itatolewa kwa mkopaji kwa kusaini mkataba utakaotayarishwa na chama ukiambatanishwa na mchanganuo wa ulipaji deni.

(f). Mikopo huu utatolewa baada ya kamati ya Mikopo kujiridhisha juu ya kuwepo kwa dhamana za uhakika zisizohamishika mf. Hati ya nyumba na Kiwanja. Nyumba isiyo na hati uthibitisho wa umiliki utatolewa na Mwenyekiti wa Mtaa.

(g). Mikopo ya biashara itatolewa mara mbili ya Akiba ya Mwanachama au Kikundi aliyochochangia.

(h). Muda wa marejesho ni miezi thelathini na sita.

6. Mikopo ya Sikukuu:-

(a). Mikopo ya sikukuu itatolewa kwa kiwango cha Tshs. 200,000/=, itatolewa wakati wa sikukuu kama X-mass, Pasaka, Idd na maulidi.

(b). Mikopo hii itapitishwa na Afisa Mikopo na kuidhinishwa na Meneja.

(c). Itarejeshwa kwa miezi miwili.

(d). Riba yake itakuwa asilimia tano na itakatwa mara moja.

6. Mikopo ya maendeleo maalumu:-

(a). Mkopo wa Maendeleo maalum utatolewa kwa kiwango kisichozidi Tshs 20,000,000/= na utatolewa mara tatu ya Akiba za Mwanachama.

(c). Mkopo huu utalipiwa Ada ya 1% kwa kiwango kinachoanzia Tshs 6,000,000/= hadi Tshs 10,000,000/=

(d). Mkopo kuanzia Tshs 10,000,001/=hadi Tshs 20,000,000/= utalipia ada ya 1% na Bima ya 1.8% kama kinga ya awali ya mkopo.

(e). Mwanachama lazima awe na hisa zisizopungua 10% ya Mkopo anaokopa.

(f). Mkopo wa Maendeleo Maalum haufutiwi na haufuti mikopo mingine.

(h). Riba ya Mkopo huu ni 2% kwa salio nyoofu(Straight line)

(i). Mikopo yote ya maratatu itatolewa kwa mkopaji kusaini Mkataba utakaotayarishwa na Chama kwa kiasi kinachoanzia Tshs 10,000,000/= ukiambatanishwa na Mchanganuo wa ulipaji wake pia lazima mkataba uthibitishwe na Mwanasheria.

(j). Mkopo huu utatolewa kwa kuzingatia historia ya urejeshaji Mikopo mingine iliyochukuliwa na Mwanachama hapo awali.

(k). Mkopo huu utatolewa baada ya kamati ya Mikopo kujiridhisha juu ya kuwepo kwa dhamana za uhakika zisizohamishika Mfano Nyumba au Kiwanja. Nyumba isiyo na hati uthibitisho wake utatolewa na serikali za Mitaa.