MADHUMUNI NA MISINGI YA USHIRIKA

Yafuatayo ni Madhumuni na Misingi ya Ushirika ya Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Tazara Mbeya SACCOS LTD

MADHUMUNI

Madhumini ya Chama hiki cha Ushirika ni kuinua na kuimarisha hali ya kiuchumi na kimaisha ya Wanachama wake kwa kufuata misingi ya demokrasia, Kanuni na taratibu za Vyama vya Ushirika kwa kuhamasisha wanachama wake kujenga tabia ya kujiwekea Akiba na kutafuta vyanzo vya Fedha ili kujenga na kuimarisha mtaji kwa ajili ya kutoa Mikopo kwa Wanachama kwa Masharti na riba nafuu. Ili kufanikisha Madhumini haya ya Ushirika huu wa Akiba na Mikopo utafanya yafuatayo:-

• Kupokea na kutunza Akiba na Amana za Wanachama kwa njia rahisi na salama.

• Kutoa Mikopo yenye Masharti nafuu kwa Wanachama yenye kukidhi mahitaji yao kiuchumi na kijamii.

• Kuwaelimisha Wanachama kujijengea tabia ya kukopa kwa busara na kutumia vizuri Mikopo kwa ajili ya kuinua hali zao za maisha.

• Kutoa bidhaa mbalimbali za fedha (Financial product) kwa Wanachama ili waweze kushiriki zaidi kuimarisha mitaji yao binafsi na kuleta mvuto kwa wasio Wanachama kujiunga na Chama.

• Kuweka kwa usalama fedha za Chama na Wanachama kwa kuanzisha mipango ya kukabiliana na majanga na/ au kuweka Bima za fedha zinazofaa .

• Kuwasaidia wanachama kuandaa mipango yao ya maendeleo katika kuwekeza mitaji kwenye miradi ya kiuchumi na huduma za jamii.

• Kutoa Elimu ya Ushirika kwa Wanachama.

• Kufanya mambo yote yale ambayo yataendeleza madhumini ya Chama.

MISINGI YA USHIRIKA

Uanachama katika Chama ni wa uwazi na hiari bila vipingamizi vyovyote. Watu wote ambao wana sifa na wako tayari kutumia huduma za Ushirika na wako tayari kutimiza wajibu wa uanachama wao wanaruhusiwa kujiunga bila kujali hali yao ya kijinsia, kijamii, mbari (racial) kisiasa, au dini yao.
Ushirka ni vyombo vya kidemokrasia vinavyoongozwa na Wanachama ambao wanashiriki kikamilifu katika kuunda sera na maamuzi, Wake kwa Waume, waliochaguliwa na wanachama wenzao, waendeshe shughuli kwa niaba ya wenzao na kuwajibika kwa wanachama wenzao. Katika Chama kila mwanachama ana haki ya kuchaguliwa kuwa kiongozi wa Chama aidha wanachama wana haki sawa ya kupiga kura (Mwanachama mmoja kura moja.
Wanachama wana haki ya kuchangia kidemokrasia mtaji wa Ushirika wao. Angalau sehemu kubwa ya Mtaji kwa kawaida inakuwa ni mali ya Ushirika. Wanachama wanatenga ziada kwa madhumini yoyote au makusudio yafuatayo; maendeleo ya Ushirika, kutenga akiba ambayo sehemu yake itagawanywa kwa wanachama kwa uwiano wa jinsi alivyoshiriki katika biashara, na shughuli nyingine zilizoidhinishwa na Wanachama
Ushirika ni Asasi huru yenye kujitegemea na kudhibitiwa na Wanachama wake. Kama zitaingia katika makubaliano na Asasi nyingine ikiwa ni pamoja na Serikali au kuupata mtaji kutoka vyanzo vya nje, zitafanya hivyo kwa Masharti amabyo yatahakikisha uongozi wa kidemokrasia wa wanachama wake na kudumisha uhuru wao.
Ushirka hutoa Elimu na Mafunzo kwa wanachama, Viongozi, menejimenti ya vyama vya Ushirika na kutumia elimu na mafunzo hayo kwa manufaa ya kuendeleza Ushirika wao. Vilevile, wataifahamisha jamii hasa vijana na viongozi kuhusu faida ya Ushirika.
Vyama vyote vya Ushirika vinawatumikia wanachama na jamii zao katika njia zilizo bora zaidi na kuimarisha shughuli za Ushirika kwa kushirikiana kuanzia ngazi ya Msingi, Mkoa, Taifa na Ki- Mataifa.
Ushirika hufanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya uhakika kwa jamii na kuzingatia Sera zilizoainishwa na wanachama wake.
Ushirka hutoa Elimu na Mafunzo kwa wanachama, Viongozi, menejimenti ya vyama vya Ushirika na kutumia elimu na mafunzo hayo kwa manufaa ya kuendeleza Ushirika wao. Vilevile, wataifahamisha jamii hasa vijana na viongozi kuhusu faida ya Ushirika.