WANACHAMA

Wanachama wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Tazara Mbeya SACCOS LTD

Utangulizi

Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Tazara Mbeya, hadi sasa kina Jumla ya Wanachama 1300 ambapo Wanaume ni 1000 na Wanawake 275 na Vikundi vya Wajasiriamali 25. Idadi ya Wanachama imeendeleo kuongezeka siku hadi siku pia Wateja wanaofungua akaunti za Amana (Current Account) wamefikia 2000. Akaunti za Amana zinazofunguliwa katika Chama chetu hazina Makato ya kila Mwezi hivyo huwasaidia sana Wajasiliamali Wadogo, Vikundi/Vikoba, Wafanyakazi na Wananchi kwa Ujumla.

Kujiunga Uanachama

Mwanachama atakapojiunga na Chama atalipa kiingilio cha Tshs 60,000/= na Hisa 100 zenye thamani ya Tshs 500,000/=. kila hisa moja itauzwa Tshs 5000, Mwanachama atatakiwa kununua hisa nne zenye thamani ya Tshs 20,000/= kila mwezi na kulipia Mchango wa Utawala wa Majanga Kiasi cha Tshs 5,000/= kila mwezi. Mwanachama aliyekamilisha kununua Hisa za Uanachama atapewa hati ya umiliki wa Hisa. Kila baada ya miaka mitano atapewa hati inayoonyesha jumla ya hisa zake za Uanachama kwa kipindi husika.

Mwombaji atakapokubaliwa

• Mwanachama atatakiwa kulipa kiingilio na Hisa za uanachama. Mwanachama atapewa kitabu cha Wanachama mara baada ya kununua kiwango kisichopungua nusu au Hisa kamili za Uanachama. Endapo kitabu cha uanachama kitapotea Mwanachama atapewa kitabu kingine baada ya kulipa kiasi cha Tshs 5000/=.

•Meneja wa Chama atarudisha Hisa na Akiba zote zilizopokelewa kutoka kwa waombaji waliokataliwa Uanachama. Ada ya fomu ya maombi na kiingilio cha Uanachama havitarudishwa.

•Wanachama wapya wataruhusiwa kupewa huduma za Mikopo mpaka watakapokuwa wamethibitishwa na Mkutano Mkuu.